Main Article Content

Abstract

Wakati huu ambao Wakenya wamechangamkia Mtaala wa Elimu wa Umilisi (CBE) kama mfumo mpya wa elimu katika shule zote za msingi za umma nchini, ipo haja ya walimu kuibua nyenzo mpya za ufundishaji, ambazo zitamlenga mwanafunzi moja kwa moja. Mojawapo ya nyenzo hizo ni matumizi ya vipera vya Fasihi ya Watoto kufundishia stadi za lugha kwa wanafunzi wa gredi za shule za msingi, yaani kuanzia chekechea hadi gredi ya sita. Fasihi ya watoto ni ile fasihi iliyoandaliwa watoto kama wapokezi na hadhira maalum. Vipera mbalimbali vya Fasihi ya Watoto vinaweza kutumiwa kufundishia wanafunzi katika gredi za shule ya msingi. Vipera hivi vinapotumiwa darasani kufundishia, wanafunzi hufaidi zaidi kwa sababu kupitia kwavyo, maarifa hupokelewa katika mwonoulimwengu wao kama watoto. Yakiongozwa na Nadharia ya Utamaduni Jamii (socio-cultural theory) ya Lev Vygotsky, makala haya yanatalii njia mwafaka za kutumia vipera mbalimbali vya fasihi ya watoto kama nyenzo ya ufundishaji wa stadi za lugha. Makala haya vilevile yameweka wazi faida ya fasihi ya watoto kama nyenzo, na kupendekeza njia zinazoweza kutumiwa ili kuepuka udhaifu unaotokana na matumizi ya vipera vya fasihi ya watoto kama nyenzo ya kufundishia. Mbinu za utafiti zifuatazo zimetumiwa kukusanya data ambayo imechanganuliwa na kuwasilishwa kama matokeo; hojaji kwa walimu, mahojiano, na utazamaji darasani, katika masomo ya Kiswahili ya shule za msingi za umma. Matumizi ya Fasihi ya watoto kama nyenzo ya kufundishia stadi za lugha yana umuhimu mkubwa kama vile kukuza stadi za lugha katika muktadha wa kijamii, kukuza uwezo wa kufikiri na tamaduni. Ili kupunguza udhaifu wa kutumia nyenzo hii utafiti umetoa mapendekezo yafuatayo: kabla ya masomo, walimu waandae mazingira ya kuelimisha, kufurahisha na kuvutia. Aidha, wachapishaji, waandishi, na mashirika ya kielimu yaendelee kukuza kazi zinazojikita katika muktadha wa Kiafrika ili kuwavutia watoto zaidi. Pia, Serikali kupitia Wizara ya Elimu pamoja na wadau wa elimu, ianzishe uundaji wa maktaba shuleni. Kando na hayo, wahakikishe kuwa maktaba hizi zimejazwa vitabu vinavyofaa kwa watoto wa umri husika.

Keywords

CBE Nyenzo Vipera vya Fasihi ya Watoto

Article Details

How to Cite
Mchango wa Fasihi ya Watoto Katika Ufundishaji wa Stadi za Lugha Katika Shule za Msingi, Mtaala wa Elimu wa Umilisi (CBE) Nchini Kenya. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(1), 24 – 30. https://doi.org/10.61889/jnwcga61

How to Cite

Mchango wa Fasihi ya Watoto Katika Ufundishaji wa Stadi za Lugha Katika Shule za Msingi, Mtaala wa Elimu wa Umilisi (CBE) Nchini Kenya. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(1), 24 – 30. https://doi.org/10.61889/jnwcga61

Similar Articles

You may also start an advanced similarity search for this article.