Main Article Content

Abstract

Makala hii inachunguza sababu za matumizi ya vipashio vya lugha vya kimamlaka na kiitikadi katika midahalo ya kisiasa ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 nchini Kenya kupitia jukwaa la YouTube. Madhumuni ya utafiti yalikuwa kubainisha namna na sababu zilizowafanya wanasiasa kutumia lugha yenye vipashio vya mamlaka na itikadi katika diskosi zao za kisiasa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Hakikifu wa Usemi (UHU) inayobainisha uhusiano kati ya lugha, mamlaka na itikadi katika jamii. Muundo wa utafiti uliotumika ulikuwa wa kiuchanganuzi wenye mkabala wa kiuthamano. Eneo la utafiti lilikuwa katika midahalo ya kisiasa ya uchaguzi wa 2022 nchini Kenya; iliyopatikana katika jukwaa la kidijitali la YouTube. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa midahalo ya wanasiasa wakuu kutoka mirengo ya kisiasa ya Azimio la Umoja na Kenya Kwanza iliyohusisha kampeni za uchaguzi huo. Data zilipatikana kwa kutumia mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ambapo video za midahalo zenye maudhui yanayodhihirisha matumizi ya vipashio vya mamlaka na itikadi zilichaguliwa kama sampuli ya utafiti. Data zilikusanywa kupitia uchunguzi wa nyaraka za kidijitali (video za YouTube), kisha zikachanganuliwa kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo kwa kuongozwa na misingi ya Uchanganuzi Hakikifu wa Usemi. Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa wanasiasa walitumia vipashio vya lugha vya kimamlaka na kiitikadi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kufichua siri za kisiasa za wapinzani, kuwalaumu wapinzani kwa matatizo ya kijamii na kiuchumi, kutoa ahadi kwa wananchi, kuwapa wananchi matumaini, kuchochea dhidi ya wapinzani na kufanikisha propaganda za kisiasa. Kwa ujumla, utafiti umeonyesha kuwa lugha ya kisiasa hutumiwa kimkakati kama nyenzo ya kudhihirisha mamlaka na kuendeleza itikadi za kisiasa kwa lengo la kushawishi mitazamo na maamuzi ya wapiga kura.

Keywords

Itikadi Malumbano Mamlaka Siasa Uchaguzi

Article Details

How to Cite
Sababu za Matumizi ya Vipashio vya Lugha vya Kimamlaka na Kiitikadi Katika Midahalo ya Kisiasa ya 2022 Nchini Kenya Kupitia Youtube: Mtazamo wa Uchanganuzi wa Kidiskosi. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(1), 40 – 49. https://doi.org/10.61889/4zbzx888

How to Cite

Sababu za Matumizi ya Vipashio vya Lugha vya Kimamlaka na Kiitikadi Katika Midahalo ya Kisiasa ya 2022 Nchini Kenya Kupitia Youtube: Mtazamo wa Uchanganuzi wa Kidiskosi. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(1), 40 – 49. https://doi.org/10.61889/4zbzx888

Most read articles by the same author(s)