Main Article Content
Abstract
Matini za kombe la dunia 2022 zilishuhudia matumizi ya ishara mbalimbali zilizobeba ujumbe muhimu kwa hadhira. Ingawa zingine zilikuwa za moja kwa moja, nyingi zilisetiri ujumbe ambao haungeweza kufasiriwa moja kwa moja na wasomaji. Lengo la makala haya ni kuchanganua matini za Kombe la dunia 2022 katika gazeti la Taifa Leo kisemiotiki ili kuweka wazi ujumbe uliolengwa. Makala imejikita katika nadharia ya semiotiki iliyoasisiwa na Saussure (1946) inayoshughulikia ishara na uashiriaji na maana zao katika matini za kifasihi na isimu. Utafiti uliofanyika ulilenga matini kuhusu kombe la dunia katika Gazeti la Taifa Leo. Sampuli ya kimaksudi ilitumika kuteua matini za kisemiotiki kwa mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo.Dta ilikusanywa kwa udurusu wa magazeti ya Taifa leo, kuchanganuliwa na kuwasilishwa kwa maelezo na madondoo ya matini za kisemiotiki. Makala inaonyesha kuwa kategoria tatu za matini za kisemiotiki za picha, maelezo na matini za kitamathali zilitumika. Ujumbe katika matini hizi ulijitokeza katika uashiriaji kisemiotiki na ulihusu uovu wa jamii (rangi nyeusi); hatari (wekundu); amani (weupe); utamu (asali), utamaduni, dini pamoja na masuala ya uchumi na biashara. Utafiti unapendekeza kuwa waandishi waimarishe sanaa na uandishi kwa kutumia mbinu na mitindo zaidi ya kisemiotiki ili kuweka wazi ujumbe wa matini za kitaaluma.
Keywords
Article Details
Copyright (c) 2026 Videlis Lusweti, Fridah Miruka, Benard Okal

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
