Uhakiki wa Masuala ya Kitamaushi Katika Riwaya ya Safari ya Lamu

##plugins.themes.academic_pro.article.main##

John Wangila
Judith Khasoa

Abstract

Waandishi wa riwaya huwasilisha masuala mbalimbali katika kazi zao. Mojawapo wa masuala  haya ni masuala ya utamaushi wa wahusika. Hali ya kitamaushi huwasilisha wakati wahusika hujiuliza kuhusu maisha, kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu duniani na kifo cha binadamu kama suluhisho la matatizo ya binadamu duniani. Tafiti za awali zilishughulikia utamaushi kama nadharia ya uhakiki na uchambuzi wa kazi za kifasihi. Ili kuelewa suala la kitamaushi zaidi, ni muhimu masuala ya kitamaushi yahakikiwe zaidi katika kazi zinazowasilisha masuala haya kiundani. Hili ndilo pengo lililochochea uandishi wa makala hii. Makala hii ilikuwa na madhumuni ya kuhakiki masuala ya kitamaushi katika riwaya ya Safari ya Lamu. Nadharia ya utamaushi ilitumiwa kuwasilisha na kuchanganua data. Riwaya ya Safari ya Lamu ilichaguliwa kimaksudi kwa sababu mwandishi alitumia wahusika waliotamauka katika kuwasilisha maudhui yake. Huu ulikuwa utafiti wa maktabani ambapo data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi yaliyomo katika riwaya husika. Kwa sababu data zilikuwa za kithamano, mbinu ya kimaelezo ilitumiwa katika uwasilishaji na uchanganuzi wa data. Makala hii ilibainisha kuwa masuala ya kitamaushi kama vile kifo, ndoa na maisha yamewasilishwa katika riwaya husika. Makala hii ni muhimu sana kwa wachanganuzi wa riwaya kwa sababu mbinu na nadharia za uchanganuzi wa riwaya ilishughulikiwa katika makala hii.

##plugins.themes.academic_pro.article.details##