Taarifa zozote za siri zitakazotolewa na mwandishi/waandishi wa makala kwa ajili ya JAKISA zitalindwa na jopo la wahariri na kutumika tu katika kufanikisha mawanda na malengo ya kitaaluma ya jarida. Taarifa hizo hazitafikiwa na mtu/watu wengineo ila jopo la uhariri wala kutumiwa kwa madhumuni tofauti; na zitaweza tu kufikia umma kwa idhini ya mwandishi/waandishi wa makala.