Jarida la Kiswahili Sanifu (JAKISA) ni jarida wazi linalotathminiwa na wenzi. Jarida hili litachapisha makala za taaluma ya Kiswahili. Makala zote zitatumwa kwa Mhariri Mkuu na kufanyiwa tathmini ya kina ya kitaaluma. Makala zitakazokubaliwa ni zile zinazotokana na tahakiki za vitabu, tasnifu, uchunguzi kifani na kazi mradi miongoni mwa nyingine. Madhumuni yake ni:

1. Kupanua welewa na ujuzi katika lugha, isimu, fasihi pamoja na utamaduni wa Kiswahili.

2. Kutoa nafasi kwa mijadala ya kitaaluma ya masuala yanayohusu Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika kwa kupokea kazi asilia kuhusu isimu, lugha, fasihi, utamaduni, historia, falsafa, mbinu za ufunzaji pamoja na taaluma zinazofungamana na Kiswahili.

3. Kutoa nafasi kwa watafiti wa Kiswahili wa viwango vya elimu ya juu kwa kupokea makala zilizoandikwa kwa Kiswahili. Hata hivyo, makala zilizoandikwa kwa Kiingereza kuhusu taaluma ya Kiswahili zitakubaliwa.