Nyimbo za Kiswahili kama mkakati wa kuhamasisha umma kuhusu UVIKO-19 nchini Kenya
##plugins.themes.academic_pro.article.main##
Abstract
Makala hii inajadili namna nyimbo zilivyotumika katika redio kuhamasisha umma kuhusu Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19). UVIKO-19 ni janga la kiafya la kimataifa ambalo lilivuruga maisha ya binadamu kote ulimwenguni. Kutokana na tishio la UVIKO-19, serikali na asasi mbalimbali zilijitolea kukabiliana na janga hili kwa kutumia mikakati tofauti tofauti ikiwemo kuhamasisha umma. Mkakati mojawapo ambao serikali ilitumia kuleta ufahamu dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona ulikuwa kutumia nyimbo za Kiswahili katika vyombo vya habari hasa redio ikichukuliwa kuwa dhima ya redio ni: kuburudisha, kuelimisha na kufahamisha. Makala hii inaonyesha namna ambavyo nyimbo hasa za kiswahili zilitumika katika redio kuhamasisha umma dhidi ya vipengele via mawasiliano ya kiafya kuhusu UVIKO-19. Inaonyesha jinsi nyimbo za Kiswahili zilivyosaidia uelimishaji na uhamasishaji wa umma dhidi ya UVIKO-19 na kuchangia pakubwa kubadili mawazo ya wananchi wa Kenya kwa njia ya burudani.
##plugins.themes.academic_pro.article.details##
This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.