Kiunzi cha Kweli-Bunilizi katika Hadithi ya “Mwendawazimu”: Mtazamo wa Uhakiki-Maeneo
##plugins.themes.academic_pro.article.main##
Abstract
Kazi za Fasihi hujikita katika kueleza hadithi za kibunilizi. Hata hivyo, katika ubunifu huu kuna uwezekano mkubwa wa kupata data za kweli kuhusu maeneo, wahusika ama maudhui. Makala hii inaangazia matumizi ya nadharia ya uhakiki maeneo katika kudadavua ukweli katika bunilizi za Kiswahili. Utafiti uliteua hadithi ya “Mwendazimu” iliyoandikwa na Shake, (2000). Ulitumia mihimili ya uhakiki-maeneo: ukiukaji mipaka, mwanda wa kijamii, mwingiliano matini na mikakati ya kiuhakiki-matini: mtazamo kwingi, mpangilio-safu na fahiwa ainati. Makala inaonyesha ufanifu mkubwa wa uhakiki-maeneo kama nyenzo ya kudadavulia ukweli katika bunilizi za Kiswahili. Mapendekezo ya utafiti huu ni kuwa mtazamo wa uhakiki-maeneo utumiwe kuchambulia hadithi nyingi ili kufaidi maarifa kutokana nao.
##plugins.themes.academic_pro.article.details##

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.