Main Article Content

Abstract

Makala hii imetathmini upokezi wa masuala ya ulemavu miongoni mwa watoto wasomaji katika hadithi teule. Katika tasnia ya fasihi kwa jumla, tafiti zinazohusiana na masuala ya ulemavu zimefanywa. Hata hivyo, tafiti nyingi za awali zimelenga; mtindo, wahusika, msigano wa majina ya ulemavu na hata semi na lugha. Aidha, katika fasihi ya watoto, tafiti za awali zimelenga mitazamo ya watoto kwa wenzao walio na ulemavu wa kimwili pekee. Ni katika msingi huu ambapo makala hii imetathmini upokezi wa masuala ya ulemavu miongoni mwa watoto wasomaji. Ili kufikia azma hii, watafiti waliwahoji wanafunzi wa gredi ya kwanza na ya pili kutoka shule za msingi Kaunti ya Kiambu. Makala hii imeongozwa na nadharia ya Mwitikio wa Msomaji ya Fish (1970). Kulingana na nadharia hii, msomaji hupokea na kufasiri kazi ya fasihi kwa njia tofauti kutegemea uzoefu wake wa usomaji, maisha na hisia zake. Data iliyochambuliwa ilikusanywa maktabani na nyanjani. Maktabani mtafiti alisoma machapisho mbalimbali kama vile makala, tasnifu na vitabu vilivyolenga mada husika. Nyanjani mtafiti aliwahusisha wanafunzi wa gredi ya kwanza na ya pili kutoka shule za msingi Kaunti ya Kiambu. Matokeo ya utafiti yalibaini kwamba maoni ya watoto wasomaji haswa kutoka SK (Shule ya Kawaida) na SJ (Shule Jumuishi) yalishahabiana kwa kiwango kikubwa baada ya kusoma na kuchambua hadithi teule. Uelewa wao wa masuala ya ulemavu ulikuwa wastani na wakati mwingine wa chini. Hata hivyo, wenzao kutoka SU (Shule ya watoto walio na Ulemavu) walionekana kuwa na uelewa wa kina kuhusiana na masuala ya ulemavu kwa kuwa wanaishi na ulemavu.

Keywords

Hadithi Masuala ya Ulememavu Upokezi Watoto wa shule za msingi

Article Details

How to Cite
Tathmini ya Masuala ya Ulemavu miongoni mwa Watoto wa Shule za Msingi. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(2), 70-80. https://doi.org/10.61889/vs9qd657

How to Cite

Tathmini ya Masuala ya Ulemavu miongoni mwa Watoto wa Shule za Msingi. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(2), 70-80. https://doi.org/10.61889/vs9qd657