Main Article Content

Abstract

Tafiti tofauti kote ulimwenguni zimegundua mtu mmoja hadi kumi kati ya 100 wanavutiwa na wahusika wa jinsia moja. Moja ya dhihirisho la mapema zaidi ulimwenguni la ushoga ni michoro ya miamba ya watu wa San Zimbabwe ambayo inaonesha mahusiano ya jinsia moja ambalo ni suala la maelfu ya miaka iliyopita. Michoro hiyo ni ushahidi wa kihistoria unaonesha kuwa ushoga umekuwepo katika bara lote la Afrika katika historia yote na haujaletwa na mataifa ya Magharibi kama inavyodaiwa na viongozi wa kiafrika. Ijapokuwa, mwelekeo wa kimapenzi kwa kawaida hujadiliwa katika makundi matatu: mpenda jinsia tofauti kuwa na mvuto kwa wahusika wa jinsia nyingine, shoga ni mwanaume anayevutiwa na wanaume wengine ilhali msagaji ni mwanamke anayevutiwa na wanawake wenzake. Kwa mantiki hii makala haya yalichunguza nafasi ya Kiswahili katika kuliweka wazi suala ibuka la LGBTQ mjini Mombasa ambako watu hawazungumzii waziwazi. Makala haya yalitumia nadharia ya Ujenzi wa Jamii ambayo inaeleza kuwa katika mwingiliano wa jamii, maarifa na mitazamo huibuka kupitia mwingiliano wa watu. Vilevile nadharia hii hueleza jinsi dhana ya kijinsia inavyoundwa na kudumishwa katika jamii. Utafiti huu ulichukua muundo wa kimaelezo na walengwa 200 walichaguliwa kimaksudi katika mji wa Mombasa. Hojaji ilitumiwa kupata data kutoka kwa walengwa hawa. Matokeo yalionesha kuwa Kiswahili kinachukuliwa kuwa chombo madhubuti cha kuhamasisha maadili ya kijamii, hasa kupitia vyombo vya habari, methali, semi, na elimu rasmi. Washiriki wengi walikubali kuwa Kiswahili kina uwezo wa kupinga tabia za LGBTQ kwa kufikisha ujumbe wa maadili na kuimarisha mshikamano wa kijamii. Hii ilionyesha kwamba Kiswahili kina nafasi muhimu katika kudumisha mitazamo ya kijinsia ya jadi na kupinga mabadiliko yanayohusiana na utambulisho wa kijinsia.

Keywords

Mabasha Mashoga Pedofila Wasenge Wasagaji

Article Details

How to Cite
Nafasi ya Kiswahili Katika Kupambana na Suala Ibuka la LGBTQ Mjini Mombasa. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(1), 31 – 39. https://doi.org/10.61889/kkcamc46

How to Cite

Nafasi ya Kiswahili Katika Kupambana na Suala Ibuka la LGBTQ Mjini Mombasa. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(1), 31 – 39. https://doi.org/10.61889/kkcamc46