Main Article Content

Abstract

Taaluma ya tafsiri inatumika kama nyenzo ya kueneza utamaduni, maarifa mapya, ujuzi, na uzoefu kutoka kwa jamii moja kwenda nyingine. Makala hii inakusudia kueleza jinsi utamaduni wa Kiafrika unadumishwa na kuhifadhiwa kupitia vipengele vya ujielezaji katika matini teule zilizotafsiriwa.  Makala hii iljikita katika uchanganuzi wa tafsiri ya riwaya ya Kaburi Bila Msalaba (1969) ambayo ni (MC1) na Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulhawali (1981) ambayo ni (MC2). Uchanganuzi huu ulipania kutoa maelezo jinsi tafsiri ya riwaya za Kareithi (MC1) na Kitereza (MC2) ambazo ni hazina ya hifadhi ya utamaduni wa Kiafrika inavyochangia na kuendeleza uhifadhi wa utamaduni kutoka lugha moja hadi nyingine kupitia udumishwaji wa vipengele vya ujielezaji. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Skopos iliyoasisiwa na Hans J. Vermeer kule Ujerumani mwaka wa 1970. Neno Skopos linatokana na neno la Kigriki lenye maana ‘nia ya kutafsiri.’ Nadharia inasisitiza kuwa kila tafsiri hutafsiriwa kwa lengo fulani na lazima litimizwe kwa kadri iwezekanavyo katika miktadha lengwa. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kusoma na kuchambua matini chanzi Kaburi Bila Msalaba na Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulhawali na matini lengwa, Unmarked Grave na Mr. Myombekere and His Wife Bugonoka, Their son Ntulanalwo and Daughter Bulihwali. Makala hii ililenga kuangazia vipengele vya ujielezaji vilivyohawilishwa kutoka utamaduni chanzi na kuingizwa kwa utamaduni lengwa na jinsi vinavyochangia uhifadhi wa utamaduni katika jamii mahususi. Mkabala wa kitaamuli ulitumika katika uwasilishaji wa data. Matokeo yalidhihirisha kwamba vipengele vya ujielezaji vimehawilishwa kutoka lugha moja kwenda nyingine hivyo basi, uhifadhi wa utamaduni umewezeshwa kupitia mchakato wa tafsiri.

Keywords

Tafsiri Uhifadhi na Skopos Utamaduni

Article Details

How to Cite
Uhifadhi wa utamaduni kupitia Udumishwaji wa Vipengele vya Ujielezaji katika fasihi: Mifano ya Tafsiri ya Riwaya za Kaburi Bila Msalaba na Bwana Myombekere Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulhawali. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(2), 18 – 25. https://doi.org/10.61889/52f3tt73

How to Cite

Uhifadhi wa utamaduni kupitia Udumishwaji wa Vipengele vya Ujielezaji katika fasihi: Mifano ya Tafsiri ya Riwaya za Kaburi Bila Msalaba na Bwana Myombekere Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulhawali. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(2), 18 – 25. https://doi.org/10.61889/52f3tt73

Similar Articles

You may also start an advanced similarity search for this article.