Main Article Content
Abstract
Tamthilia kama mojawapo ya tanzu za fasihi andishi ni kioo cha jamii. Hii ni kwa misingi kwamba tamthilia huelimisha jamii kuhusu mila na tamaduni zinazoelekeza mahusiano ya wanajamii, maendeleo, mazingira, uongozi na mengineyo. Elimu ipatikanayo kupitia fasihi husawiri muono ulimwengu wa jamii husika. Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa pamoja na kuwa maendeleo ya vijana katika jamii yanawiana na uhusika wao katika kuikuza jamii, ni tafiti chache ambazo zimelenga nafasi na uhusika wa vijana katika fasihi ya Kiswahili. Ni kutokana na ukweli huu ambapo makala hii inachanganua sauti za vijana wa kike na wa kiume kuhusu mabadiliko ya kijamii katika tamthilia za Mstahiki Meya (Arege, 2009) na Bembea ya Maisha (Arege, 2022) za Timothy Arege. Makala hii inajikita kwenye: dhamira, maudhui, lugha na wahusika (uhusika) vijana wa kike na wa kiume. Kazi hii itaongozwa na mihimili ya nadharia ya uhalisia. Tamthilia hizi ziliteuliwa kimaksudi kwa kuzingatia kuwa mwandishi ni wa karne ya 21. Kazi hizi zimeangazia masuala yanayowakumba vijana kwenye karne 21. Aidha, tamthilia hizi zimekuwa zikitahiniwa katika mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne (KCSE) nchini Kenya pamoja na kuigizwa katika majukwaa mbalimbali. Hili limefanya tamthilia hizi kuwa chachu na kuwapevua mawazo yao kuhusu jamii wanamoishi. Utafiti huu ulikuwa wa kiuthamano. Njia ya ukusanyaji wa data ilikuwa ni kuhakiki matini na upitiaji wa nyaraka maktabani. Malengo ya makala hii ni kubainisha sauti ya vijana kuhusu mabadiliko ya kijamii katika kazi zilizoteuliwa. Kazi hii itakuwa mchango katika ulingo wa fasihi, elimu, wasomi wanaoshughulikia masuala ibuka katika jamii na jamii kwa jumla.
Keywords
Article Details
Copyright (c) 2026 Roseline Mwikali Kasuma, Riro Matinde Samwel

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
