Main Article Content

Abstract

Tangu kuasisiwa kwa nadharia hii ya fasihi mazingira mwaka wa 1996 na Cheryl Glotfelty, watafiti na wahakiki wengi wa fasihi mazingira wamekuwa na tashwishi ya kuitumia katika uchanganuzi na uhakiki wa kazi zao. Hii ni kwa sababu nadharia hii imeonekana kuwa pana mno, na inayokosa mawanda maalumu na bayana. Baadhi ya wahakiki wamedai kwamba nadharia hii si ya kifasihi kwa sababu inaonekana kulazimishiwa katika fasihi. Hata hivyo, baadhi ya wataalamu waliowahi kutumia nadharia hii kama vile Glotfelty na Fromm kwa ustadi mkubwa wanaikolezea sifa kwa madai kwamba licha ya upana wake, kila mhakiki na mtumiaji wa nadharia hii ndiye wa kuamua jinsi atakavyoitumia katika utafiti wake. Kazi hii kwa hivyo, inachochewa na mjadala huu wa kuunga na kupinga matumizi ya nadharia hii katika fasihi, kwa lengo la kuonyesha mawanda yake halisi na kutoa maelekezo ya matumizi. Katika kutekeleza hili, kazi hii itatalii machapisho ya wataalumu mbalimbali waliowahi kuchangia mawanda na matumizi ya nadharia ya fasihi mazingira tangu kuasisiwa kwake mwaka wa 1978 hadi 2022. Aidha, utafiti utajaribu kuonyesha mawanda ya nadharia hii katika fasihi ya Kiswahili, kwa kurejelea machapisho yaliyowahi kuwasilishwa au kuchapishwa kuhusu fasihi ya Kiswahili. Aodha, mchango wake mkubwa umo katika kukusanya matapo au mirengo yake mbalimbali katika chapisho la Kiswahili linaloweza kutumiwa kama marejeleo.

Keywords

Fasihi Mazingira Nadharia Uhakiki

Article Details

How to Cite
Nadharia ya Fasihi Mazingira: Mawanda na Matapo yake Katika Fasihi ya Kiswahili. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(1), 9 – 14. https://doi.org/10.61889/je3p5b16

How to Cite

Nadharia ya Fasihi Mazingira: Mawanda na Matapo yake Katika Fasihi ya Kiswahili. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(1), 9 – 14. https://doi.org/10.61889/je3p5b16