Main Article Content
Abstract
Makala hii inaangazia uhusiano kati ya lugha ya Kiswahili na utekelezaji wa huduma za Teletiba katika hospitali za Kaunti ya Murang’a, Kenya. Teletiba inazidi kutumika kama njia mbadala ya kutoa huduma za afya katika maeneo ya mashambani na yaliyo mbali na vituo vikubwa vya matibabu. Ufanisi wake unategemea uwezo wa wahudumu wa afya na wagonjwa kuwasiliana kwa ufasaha. Kwa kuzingatia Kiswahili kama lugha rasmi na ya taifa nchini Kenya, utafiti huu ulichunguza jinsi matumizi yake yanavyoathiri upatikanaji, ufanisi na uendelevu wa huduma za Teletiba.
Nadharia ya Matumizi na Kuridhika (Uses and Gratifications Theory - UGT) ilitumika kueleza sababu za wagonjwa na wahudumu wa afya kutumia Teletiba. Mbinu ya utafiti wa nyaraka ilitumika, ambapo nyaraka 20 zilizochaguliwa kwa makusudi zilichambuliwa ili kubaini mada, mawazo na taarifa muhimu kuhusu Teletiba na matumizi ya Kiswahili. Uchambuzi ulilenga kuelewa nafasi ya lugha katika mawasiliano ya afya na matumizi ya huduma za kidijitali. Matokeo yalionyesha kuwa Kiswahili kina jukumu muhimu katika kuwezesha mawasiliano kati ya watoa huduma za afya na wagonjwa, kuboresha uelewa wa masuala ya afya na kuongeza ushiriki wa wagonjwa katika maamuzi ya matibabu. Matumizi ya Kiswahili pia yalijenga uaminifu, ukaribu na uelewa wa kiutamaduni kati ya wagonjwa na wahudumu wa afya. Hata hivyo, changamoto zilibainika, zikiwemo uhaba wa rasilimali za Teletiba kwa Kiswahili na ukosefu wa wataalamu wanaotoa huduma kwa lugha hiyo. Kwa upande mwingine, utafiti wa bunilizi za Kiswahili ulitumia nadharia ya uhakiki-maeneo kuchambua ukweli katika hadithi ya “Mwendazimu” iliyoandikwa na Shake (2000). Matokeo yalionyesha kuwa nadharia ya uhakiki-maeneo ni nyenzo muhimu ya kudhihirisha ukweli katika bunilizi za Kiswahili. Utafiti unapendekeza kuimarishwa kwa Kiswahili katika Teletiba na matumizi ya uhakiki-maeneo katika uchambuzi wa bunilizi.
Keywords
Article Details
Copyright (c) 2026 Harrison Gatuthu Muiga, Jacktone Onyango, Jackline Murimi

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
