Main Article Content
Abstract
Nafasi ya mwanamke katika jamii imeendelea kuwa muhimu kila siku. Mathalani watunzi wa kazi mbalimbali za fasihi wakiwemo wa ushairi wameendelea kumsawiri mwanamke katika kazi zao. Aidha, wahakiki wa kazi mbalimbali za fasihi wanaonesha kuwa diwani mbalimbali zilizotungwa hususani na watunzi wakiume, zimemsawiri mwanamke kwa mtazamo duni. Makala hii inalenga kuchunguza usawiri wa mwanamke katika diwani iliyotungwa na mtunzi mwanamke. Data za makala hii zilipatikana katika Diwani ya Kurunzi ya Rose Mbijima kwa mbinu ya usomaji makini. Matokeo yanaonesha kuwa yapo maendeleo makubwa yaliyopigwa na mwanamke katika kujiondoa katika hadhi ya chini na hali duni, kama ambavyo anachorwa katika kazi nyingi za kifasihi. Data zinadhihirisha kuwa mtunzi amemchora mwanamke kwa kiasi kidogo katika mtazamo hasi hususani katika masuala ya mapenzi na ndoa kuakisi hali ilivyo katika jamii nyingi za kiafrika. Aidha, mtunzi mwanamke amemsawiri mwanamke katika mtazamo chanya kwa kiwango kikubwa. Mwanamke amesawiriwa kama mtu mwenye mtazamo wa kimapinduzi juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea katika jamii, mwanamke ameonekana akipaza sauti na kutoa maoni yake. Makala hii, inahitimisha kwa kutoa mapendekezo kuwa, kazi za watunzi wa kike wa ushairi ziendele kutafitiwa ili kuchochea mabadiliko makubwa ya wanawake juu ya mtazamo hasi dhidi ya jinsi yao na jamii kwa ujumla kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii.
Keywords
Article Details
Copyright (c) 2026 Davian Buguna

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
