Main Article Content
Abstract
Makala imechunguza namna waandishi wa kike nchini Kenya na Tanzania wanavyowasawiri wahusika wa kiume. Kwa kutumia mkabala linganishi, riwaya mbili za waandishi wa kike wa Kenya Tumaini (Momanyi, 2006), Dago wa Munje (Ryanga, 2008) na za Tanzania Kipimo cha Mizani (Burhani, 2004) na Hiba ya Wivu (Mwanga, 1997) zimechunguzwa. Kwa kuwa taswira za wanaume katika kazi za fasihi zilizoandikwa na wanawake zimetafitiwa kwa uchache sana mkabala linganishi wa waandishi wanawake wa nchi mbili tofauti haujatumika kabisa. Pengo hili limezibwa na makala hii. Waandishi wanaandika kazi zao na kuonesha tawira juu ya jinsia fulani kulingana na taasubi zilizowakuza. Jambo hili huonesha utofauti baina ya mtunzi mmoja na mwingine. Makala hii imejikita kwenye nadharia za uhalisia ujifunzaji wa kijamii iliyo na misingi kwenye uana na nadharia ya mwanaume mpya. Kutokana na uhakiki, wahusika wa kiume wamesawiriwa kwa njia hasi na chanya na waandishi wanawake. Taswira zao hasi ni kama walevi, wababe, wavivu, katili, wadanganyifu na wenye maringo, wapenda rushwa, wadhulumaji, wakorofi, wenye tamaa na washari. Taswira chanya wanazoziibua waandishi wanawake kuhusu wahusika wa kiume ni: wenye bidii, wachapakazi, wenye upendo na mshikamano kwa kujitoa kwa ajili ya wengine, wakweli na wawazi. Taswira hizi zinaibuliwa na waandishi kulingana na walivyoichunguza jamii husika. Lengo la waandishi kuyaweka bayana haya ni kutaka jamii ibadilike na kuwa na matendo mema na mazuri hasa kwa hao wahusika wa kiume tuliowaangazia katika makala hii.
Keywords
Article Details
Copyright (c) 2026 Olivia Kanwa

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
