Main Article Content
Abstract
Makala hii inaangazia jinsi kizazi cha Gen Z hubuni upya methali asilia za Kiswahili kwa kuongeza au kubadilisha maneno ili ziwiane na uhalisia wa miktadha ya sasa. Hali hii hupoteza jgmaana zilizokusudiwa za methali asilia pamoja na uzito wa hekima iliyomo. Mabadiliko hayo huibua ucheshi na kukejeli hekima ya pamoja ya jamii. Kwa misingi hii, makala imechunguza jinsi ubunifu huo mpya unavyosababisha mabadiliko ya maana, maneno yaliyomo na kuongeza vifungu vya maneno katika methali za kimapokeo ili ziwiane na miktadha mipya zinamotumika. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Baada-Usasa kwa mujibu wa Lyotard (1984). Muundo wa utafiti ni wa kimaelezo. Eneo la utafiti ni mtandao wa kijamii wa Tiktok, Kenya na eneo la kitaaluma ni fasihi simulizi. Data za msingi zilikusanywa kwenye mtandao wa kijamii wa Tiktok, Kenya na maktabani ambako data za upili zilikusanywa. Sampuli ya utafiti ni baada-methalijadi za Kiswahili. Baada-methalijadi 20 zilikusanywa. Baada-methalijadi 8 ziliteuliwa kimaksudi na kuchunguzwa. Data za methali za kimapokeo zilichanganuliwa pamoja na kila baada-methalijadi iliyotokana nazo. Mabadiliko ya kimaana, kimuundo na kimuktadha ya kila methali yalijadiliwa huku watafiti wakirejelea maoni ya watafiti wengineo kuhusu methali hizo mpya. Matokeo ya utafiti yalifichua kuwa vijana wa kizazi cha Gen Z hubadilisha muundo na maana za methali za kimapokeo ili kukidhi haja za uhalisia wa miktadha ya sasa.
Keywords
Article Details
Copyright (c) 2026 Lina Akaka, Mugwe Mwaniki

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
