Main Article Content

Abstract

Kila msanii huwa na upekee wa kimtindo katika kuisuka kazi ya fasihi na vilevile wasanii tofauti aghalabu huandika kazi zao katika awamu tofauti za kihistoria na kiwakati.  Licha ya haya, mwingiliano wa namna fulani huelekea kutokea kati ya kazi husika za kisanaa za wasanii. Hivyo basi, makala hii inatathmini mwingilianomatini kati ya riwaya ya Utubora Mkulima (Shaaban, 1966) na Siku Njema (Walibora, 1996) huku ikiongozwa na nadharia ya Mwingilianomatini iliyoasisiwa na Julia Kristeva (1980) na kuendelezwa na wataalamu kama vile Allen, Mikhail Bakhtin na Ferdinand De Saussure. Data za kazi hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya udurusu wa makala za kitaaluma maktabani. Uchambuzi wa data ulifanywa kupitia mbinu ya uchambuzi wa kimaudhui. Utafiti huu umebainisha kuwa kuna mwingiliano wa kisifa baina ya wahusika katika riwaya hizi mbili kama vile sifa ya upweke, bidii, uadilifu, uwerevu na utajiri. Aidha, kuna mwingiliano kimaudhui kuhusu kazi hizi mbili kama vile kazi, mapenzi na kifo. Utafiti huu utawasaidia wanachuoni katika kuelewa na kuangalia kazi za nyanja nyinginezo za kifasihi kimwingilianomatini.


 

Keywords

Mwingiliano matini Maudhui Riwaya Wahusika

Article Details

How to Cite
Mwingilianomatini katika Riwaya za Siku Njema na Utubora Mkulima. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(2), 130-139. https://doi.org/10.61889/9gsfd446

How to Cite

Mwingilianomatini katika Riwaya za Siku Njema na Utubora Mkulima. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(2), 130-139. https://doi.org/10.61889/9gsfd446

Similar Articles

You may also start an advanced similarity search for this article.