Main Article Content

Abstract

Makala hii inachunguza usawiri wa mhusika Fatuma kama kielelezo cha mwanamke shujaa wa Kiislamu katika Utenzi wa Fatuma. Madhumuni ya makala hii ni kubainisha namna mhusika Fatuma anavyowakilisha ushujaa wa mwanamke katika muktadha wa Kiislamu na jinsi anavyotumika kama mfano wa kuigwa na wanawake. Makala hii imetumia ufeministi wa Kiislamu kama kiunzi cha nadharia.Muundo wa kiuthamano unaojumuisha mbinu ya uhakiki wa matini ndiyo iliyotumika kukusanya na kuchanganua data ya utafiti. Data inayochanganuliwa inatokana na maelezo kutoka kwa Utenzi wa Fatuma.Matokeo ya makala hii yanaonyesha kuwa mhusika Fatuma amesawiriwa kuwa mtiifu kwa baba yake na mume wake, mwadilifu, mwaminifu katika ruwaza za dini ya Kiislamu, mwenye rajua ya kuwa mwombezi na mtetezi wa wanawake Waislamu siku ya kiyama, na jasiri. Kutokana na sifa zifa hizi, makala hii inadhukuru kuwa, mhusika Fatuma ni mfano wa mwanamke shujaa ambaye kwa kujitolea kwake katika dini, familia, na jamii, anaendeleza haki, usawa, na ustawi wa wanawake Waislamu. Aidha, mhusika Fatuma anawakilisha nafasi muhimu ya wanawake katika fasihi ya Kiswahili, usawiri wake ukichangia katika kukuza uelewa wa mkabala wa ufeministi wa Kiislamu na kujenga mtazamo mpya kuhusu usawiri wa wanawake katika utenzi. Makala hii inatoa mchango muhimu katika utafiti wa fasihi ya Kiswahili kwa kuangazia mwingiliano kati ya fasihi, dini, na uana, na hivyo kubainisha namna vipengele hivi vinavyoshirikiana katika kujenga na kuimarisha taswira na nafasi ya wanawake katika jamii.

Keywords

Haki Shujaa Ufeministi wa Kiislamu Usawa Utenzi

Article Details

How to Cite
Usawiri wa Fatuma kama Kielelezo cha Mwanamke Shujaa wa Kiislamu katika Utenzi wa Fatuma. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(2), 1-9. https://doi.org/10.61889/h1g89q78

How to Cite

Usawiri wa Fatuma kama Kielelezo cha Mwanamke Shujaa wa Kiislamu katika Utenzi wa Fatuma. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(2), 1-9. https://doi.org/10.61889/h1g89q78