Main Article Content

Abstract

Makala hii inachunguza jinsi miviga inavyoathiri jamii kwa kuangazia umuhimu wa Miviga katika jamii na matatizo yanayoikumba miviga. Inalenga kubainisha athari za miviga katika jamii ya Kitanzania hasa kabila la wamakonde wa Newala mkoa wa Mtwara katika kipindi cha utandawazi. Maandiko ya wataalamu mbalimbali yamepitiwa ili kubaini kuathiriwa na kuathiri kwa miviga katika jamii za binadamu. Uchunguzi ulifanyika mkoani Mtwara wilaya ya Newala katika kata ya Julia. Vijiji mbalimbali viliyoko katika kata hiyo vimehusika ambapo watafitiwa hamsini (50) kutoka rika zote wametumika katika uchunguzi huu. Data za msingi zilikusanywa kutoka uwanjani kwa kutumia mbinu mbalimbali kama mahojiano, hojaji, ushuhudiaji na ushiriki. Data za upili zilipatikana maktabani kwa kusoma vitabu na tafiti mbalimbali vinavyohusiana na mada hii. Vilevile uchambuzi na uchanganuzi wa data ulifanyika kwa kutumia mbinu ya kiidadi na isiyo kiidadi. Kutokana na uchunguzi huu imethibitishwa kuwa miviga katika jamii ina umuhimu kama vile kuelimisha, kudumisha utamaduni, kuleta jamii pamoja, kuwatahadharisha watu wajiepushe na mikosi na kuburudisha jamii. Pia sherehe za miviga husababisha matatizo mbalimbali katika jamii kama mimba za wasichana wenye umri mdogo, kuongezeka kwa wategemezi, maradhi, ukosefu wa elimu ya afya na kuacha shule. Kutokana na data za nyanjani zinaonesha kuwa suluhisho la matatizo haya ni; elimu kwa jamii, sheria kwa wakiukaji na kuboresha utamaduni kuendane na wakati ni mambo ya msingi katika kupunguza athari za miviga katika jamii ikiwemo jando na unyago. Mwisho makala hii, imetolewa mapendekezo kwa jamii kwa kutoa msisitizo wa kutoa elimu kwa wanajamii. Elimu ni juu ya jinsi ya kuepuka mila zilizopitwa na wakati pamoja na kudumisha tamaduni zenye faida kwa kurekebsha baadhi ya mila ziende na wakati. Mila za kuboresha ni kama vile kuongeza umri wa vijana na mabinti kufanyiwa sherehe za miviga kama vile jando na unyago. Vilevile serikali inafaa kufuatilia wazazi wanaopotosha watoto wao kutoendelea na shule kisa sherehe za miviga ikiwemo maandalizi yake.

Keywords

Athari Jamii Miviga Utamaduni Utandawazi

Article Details

How to Cite
Athari ya Miviga Katika Jamii ya Wamakonde Kama Kielelezo cha Utamaduni Zama za Utandawazi: Wilayani Newala Mtwara Tanzania. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(1), 15 – 23. https://doi.org/10.61889/1vck0s23

How to Cite

Athari ya Miviga Katika Jamii ya Wamakonde Kama Kielelezo cha Utamaduni Zama za Utandawazi: Wilayani Newala Mtwara Tanzania. (2026). Jarida La Kiswahili Sanifu, 3(1), 15 – 23. https://doi.org/10.61889/1vck0s23