Main Article Content

Abstract

Ili mtaala wa elimu uweze kutekelezwa kwa njia inayofaa, ni muhimu kubaini mielekeo ya wadau husika. Hii ni kwa sababu mielekeo husaidia kujua mtazamo wao kuhusu mtaala huo, sababu za mielekeo yao na mikakati kuwekwa ili kuhakikisha mtaala unatekelezwa vilivyo. Walimu na wanafunzi ni baadhi ya wadau wanaohusika katika utelekezaji wa mtaala. Katika Mtaala wa Umilisi, Kiswahili ni somo la lazima linalofundishwa katika shule ya msingi. Ufundishaji wake unahusu wanafunzi kufanya mazoezi wakielekezwa na walimu, lengo likiwa ni kujenga umilisi wao katika lugha ya Kiswahili. Tafiti zimeonyesha kuwa walimu wana umuhimu kwa wanafunzi kwani hutagusana na wao sana shuleni. Inatarajiwa walimu wanaofundisha somo la Kiswahili watakuwa na athari chanya au hasi kwa mielekeo ya wanafunzi, suala ambalo makala haya yalitaka kubaini. Nadharia ya Kitendo Kinachofuata Mantiki ya Ajzen & Fishbein (1980) iliongoza makala haya. Data ilikusanywa kupitia ushuhudiaji miongoni mwa wanafunzi wa gredi ya tatu kutoka shule ishirini zilizoteuliwa kimaksudi katika gatuzi dogo la Masaba Kusini, kaunti ya Kisii. Ilibainika kuwa wanafunzi walikuwa na mielekeo chanya na hasi kuhusu Kiswahili kutegemea namna walivyofundishwa na walimu wao. Pia, kuna wanafunzi ambao walionyesha unasibu katika mielekeo yao. Makala haya ni muhimu kwani yatawasaidia walimu kufahamu athari yao kwa wanafunzi na kuboresha ufundishaji wao wa Kiswahili katika Mtaala wa Umilisi.

Keywords

Mielekeo Mtaala wa Umilisi Ufundishaji Ufundishwaji

Article Details

How to Cite
Mbinu Zinazozua Mielekeo ya Wanafunzi katika Ufundishwaji wa Kiswahili katika Mtaala wa Umilisi: Mfano wa Gatuzi Dogo la Masaba Kusini. (2025). Jarida La Kiswahili Sanifu, 2(2), 19 – 25. https://doi.org/10.61889/jakisa.v2i2.119

How to Cite

Mbinu Zinazozua Mielekeo ya Wanafunzi katika Ufundishwaji wa Kiswahili katika Mtaala wa Umilisi: Mfano wa Gatuzi Dogo la Masaba Kusini. (2025). Jarida La Kiswahili Sanifu, 2(2), 19 – 25. https://doi.org/10.61889/jakisa.v2i2.119