Matumizi ya mkabala njia mseto katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za upili
##plugins.themes.academic_pro.article.main##
Abstract
Maandalizi ya walimu huangazia vipengele mbalimbali ili kufaulisha ufundishaji unaofaa. Mojawapo ya vipengele hivi ni matumizi ya mkabala njia mseto katika ufundishaji ili kuimarisha uelewa wa wanafunzi. Licha ya hali hii, walimu wengi hupendelea kutumia mbinu moja ambayo hukuruza uelewa wa mada husika na hivyo kuathiri matokeo katika somo la Kiswahili. Lengo la makala hii ni kudadavua matumizi ya mkabala njia mseto katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili. Makala imejikita katika nadharia ya Mawasiliano iliyoasisiwa na Hodge & Kress (1988) na kuendelezwa na Kress (2010) na muundo wa usoroveya fafanuzi. Utafiti uliohusika ulilenga walimu na wanafunzi wa kidato cha tatu katika shule za upili za upeo za Kaunti ya Kakamega. Makala inaonyesha kuwa walimu wengi (80%) hutumia mkabala njia mseto katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiswahili. Walimu wana ufahamu wa njia za mawasiliano na mbinu za kufundisha ila hawana ufahamu kuwa wanapotumia njia za mawasiliano na mbinu za kufundisha wanashirikisha mkabala njia mseto. Makala hii ilihitimisha kuwa matumizi ya mkabala njia mseto huongeza motisha, huvuta umakinifu na huhakikisha ufanisi katika somo la Kiswahili. Makala inapendekeza kuwa mkabala njia mseto utumike ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili. Vilevile warsha, semina na symposia kuhusu mkabala njia mseto kwa walimu wa Kiswahili katika shule za upili ziandaliwe ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kwa mkabala njia mseto.
##plugins.themes.academic_pro.article.details##
This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.